ads

MVUA kubwa iliyoambatana na upepo iliyonyesha kwa dakika 30 imesababisha kifo cha mtoto mmoja na watu wengine watano kujeruhiwa, huku ikibomoa nyumba zaidi ya 20 na vyumba vitatu vya Shule ya Msingi Idilo, wilayani Mpwapwa.


Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri amethibitisha, akisema mtu huyo alikufa baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba.

Amemtaja aliyekufa kuwa ni Msafiri Erasto (9), mkazi wa Lukole wilayani hapa. Aidha amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Yared Msenzi (60) Siwatu Delela, Alex Delela na Tumayo Msenzi (50).

Mvua hiyo ilinyesha juzi Januari 3 na kwamba majeruhi ni watu wa familia moja.

Mkuu huyo wa wilaya ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama amesema kwamba majeruhi wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Benjamini Mkapa.

Aidha, amesema wameunda kamati ya tathmini kuona athari zilizosababishwa na mvua hiyo.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Boniface Makiya alisema wanajipanga kurejesha vyumba vya madarasa katika hali ya kawaida ili viweze kutumika kuanzia jumatatu ijayo.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: